Artists News in Tanzania

Q Chilla:Starehe, Madawa ya Kulevya Yamenipotezea Muda Sana

KIRAKA wa muziki wa Bongo Fleva  Abubakary Katwila ‘Q chief’ ambaye aliwika sana  mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa na kibao chake cha ‘Ulinizaa wewe’ ambacho kilivuta sana hisia za wababa wengi ambao wanatabia ya kukataa watoto wao.

‘Q chief’

Wimbo huo ulikuwa kama wimbo wa Taifa awe mkubwa mtoto lazima auimbe ulifanikiwa kumbamba vituo mbalimbali vya redio kwa siku ulikuwa ukisikika  hata mara kumi kila mtangazaji, aliyekuwa akiingia basi alikuwa akiupiga.

Hakuishia hapo alizidi kupiga vibao vikali vingi na akawa nembo ya  kiitikio wasanii wengi wakongwe na wachanga walihitaji kufanya nae colabo  na alikuwa akisimama kwenye kiitikio basi lazima wimbo uhit.

Qchilla kama ambavyo anapenda aitwe sasa, anasema isingekuwa kujiingiza katika uvutaji wa madawa ya kulevya sasa hivi nadhani angekuwa kwenye levo ya kimataifa kwa kuwa alikuwa ndiye msanii aliyekubalika sana Afrika Mashariki na wapo wasanii wengi ambao sasa hivi wanafanya vizuri amewasaidia kutoka au wamefuata nyayo zake.

“Nashukuru Mungu nimeachana kabisa na dawa za kulevya sikushinikizwa na mtu niliamua mimi mwenyewe kwa kuona muelekeo wangu wa maisha umepotea  nimekuwa sio mimi tena ambae nilikuwa na uwezo wa kutoa wimbo mpya hata kila wiki, sihitaji kumlaumu mtu yeyote yule nahitaji kuanza upya na kusonga mbele kwa sababu nafasi yangu ipo.”

MENEJIMETI NA DAWA ZA KULEVYA KWA WASANII

Q Chief anadai kuwa kuna baadhi ya Meneja ndio ambao wanawafikisha katika halii hii wasanii na yote inatokana na mikataba mibovu huku kazi unayofanya ni kubwa tofauti na  unacholipwa.

“Kwa kweli  meneja wengi ndio wanaosababisha wasanii wengi kujiingiza katika dawa za kulevya kwa kuwafanyika kazi kubwa tofauti na malipo na hii yote imetokana na meneja hao kuwa watu wenyepesa, ila nampongeza sana mdogo wangu Diamond amefanikiwa kwa kuwa yeye sasa ndio amemuajiri meneja na wote tukifikia huko basi wasanii wengi tutatoka.”

Aidha ameongeza kuwa kama mtu anahitaji kumsimamia amsimamie sio kumdhulumu kwa kutumia pesa zake na kumpotezea malengo yake hicho kitu huwa kinaniumiza sana ila namshukuru sana Mungu hapa nilipofika.

KWELI NAFASI YAKE IPO

Ni kweli sasa hivi tumetambulika kimataifa na nawapa sana Hongera Ally Kiba na Diamond kwa kufanikisha hilo, ila kati ya wasanii wote waliopo bado hawajakava nafasi yangu na ndio maana nasema bado ipo na mwenyewe nimerudi.

“Ukweli ninaladha tofauti sana angalia nilipotoa Mdogo mdogo  nikaja na Mungu wa Ndizi na sasa ni Koku hapo ndipo utakapoamini kuwa nafasi yangu ipo, na sidhani kama safari hii nitaiachia.”

Nimejizatiti sana hasa ukiangalia wimbo wangu huu wa Koku niliomshirikisha  Patorankig kutoka Nigeria, nimefanya kweli na ninauhakika nitairudisha heshima yangu na kuupa hadhi muziki wa kizazi kipya kama nilivyoanza.

 

KOKU IMEFANYIKA NCHI TATU

Wimbo wa Koku tumeufanyia kwenye nchi tatu tofauti ili kupata ladha ya Kiafrika zaidi na ubora wa vichwa vitatu naimani itaonyesha utofauti kwani tangu na anza muziki mimi ni mtu wa tofauti sana na ninauwezo wa kipekee.

“Kama Tanzania nilishawahi fanya video zake, South Afrika pia, nimeamua sasa kuweka ladha za Nigeria ili kuleta utamu hivyo kazi hii imefanyika Nigeria, Tanzania na South Afrika, watanzania waaitafute ili waone  Chilla wa sasa na wazamani.”

USHAURI

Nawashauri vijana kuwa makini na dawa za kulevya kwani ndio kitu ambacho kinakupotezea malengo ya maisha, watanzania wengi walitarajia ndio niwe wa kwanza kuwika kimataifa lakini ujana ulinidanganya tusiuendekeze ujana.

Pia kwa wasanii ambao wameshajiingiza katika dawa za kulevya wanachotakiwa kufanya nikujikubali na kuikataa hali ya uvutaji kwa kufanya hivyo basi wataweza.

“Mimi nilikataa mwenyewe na nikakubali matibabu, sasa ukimchukua mtu na kumpeleka kwenye matibabu wakati yeye mwenyewe bado hajakubali matokeo itakuwa ngumu na itakuwa kama mchezo wa kuigiza atacha kwa muda na baadae atarudia tena .”

Mtanzania

Comments

comments

Exit mobile version