Queen Darleen Afichua Kinachoibeba WCB
MWANADADA pekee kutoka kundi la WCB, Mwajuma Abdul ‘Queen Darling’, amesema kundi hilo limekuwa likifanya vizuri kutokana na umoja na nidhamu waliyojiwekea.
Akizungumza na MTANZANIA, Queen Darling ambaye ni dada wa kiongozi wa lebo hiyo ya Diamond Plutnumz, amesema wasanii wa kundi hilo kila mtu anaelewa dhumuni la kuwepo hapo na ndio maana hawajawahi kutetereka tangu kundi lianzishwe.
“Ni sheria ambazo wenyewe tunajiwekea hasa malengo yetu ya kuhakikisha tunatimiza kile tulichokusudia, kikubwa nidhamu tumeipa kipaumbele sana na ndio maana hujawahi kusikia Wasafi wana tatizo lolote na mtu,” alisema.
Alisema wamekuwa wakifanya ushindani wa kimaendeleo ambao umezidi kuwapa motisha ya kufanya kazi, huku kila mmoja akijiona ana deni kubwa ndani ya kundi hilo.