Artists News in Tanzania

Quick Rocka na Siri ya Kugandana na Kajala

GEMU la Muziki wa Bongo Fleva lina vijana wengi wenye vipaji,  miongoni mwao ni Abbott Charles ‘Quick Rocka’ aliyeanza kusikika mwishoni mwa miaka ya 2000 akiwa na Kundi la The Rockers.

Kundi hilo liliundwa na wasanii Mo Rocka, Chief Rocka na Dau Rocka waliotamba na ngoma ya The Rockers Antherm. Ungana naye katika Exclusive interview na gazeti hili.

Uwazi Showbiz: Vipi kuhusu kazi Quick? Ukweli ni upi juu ya ngoma mpya ya Hapo, nani mmiliki?

 Quick Rocka: Kazi zinasonga kama kawa, ngoma ya Hapo tunamiliki wote ambao tumeimba. G Nako ana haki nayo na hata Jux, so haina mmiliki mmoja.

Uwazi Showbiz: Katika studio yako ya Switch Records kuna wasanii ambao umewasaini au inafanyaje kazi?

Quick Rocka: Hakuna msanii niliyemsainisha lebo, msanii yeyote anayehitaji kufanya kazi analipia gharama atakazotakiwa kutoa, lakini mipango ya kusainisha wasanii lebo ipo japo kwa sasa nimewekeza nguvu kumsimamisha kwanza Prodyuza Luffa ili akipata jina iwe rahisi kupiga kazi na wasanii mbalimbali.

Uwazi Showbiz: Inakuwaje katika ‘charges’ kwa wasanii kufanya ngoma?

Quick Rocka: Inategemea na jina la msanii. Kama bado ni chipukizi tunawafanyia bei ndogo kwa sababu tunafahamu bado muziki si biashara yao ya kuwaingizia kipato, lakini kwa wasanii wenye majina gharama ziko juu na siwezi kuzianika hapa kwa sababu za kibiashara.

Uwazi Showbiz: Kundi lenu vipi, ndiyo limekufa au kuna nini kinaendelea?

Quick Rocka: Dah! The Rockers bwana kila mtu anafanya ishu zake. Dau anajihusisha na masuala yake ya kibiashara, Chief ameajiriwa, Mo Rocka anakomaa na gemu sometimes, mimi ndiyo kama hivi! So kundi lipo lakini kila mtu yuko bize na ishu zake.

Uwazi Showbiz: Vipi kuhusu uhusiano wako na Kajala pamoja na hizi ishu zinazoendelea kuwa anatoka na watu wengine?

Quick Rocka: Mambo ya Kajala aachiwe Kajala. Link yangu mimi na yeye haihusiani kabisa na mambo yake ya kawaida. Kitu ambacho wengi hawakifahamu uhusiano wetu uko kishikaji so kama yeye ana mtu mwingine fresh tu, sina tatizo.

Uwazi Showbiz: Wasanii wengi kwa sasa wanakomaa kupiga kazi watoke kimataifa, Vipi wewe?

Quick Rocka: Mipango ipo, niko katika mazungumzo na Wizkid pamoja na Mapholisa wa Sauz.

Uwazi Showbiz: Nakushukuru sana Quick, lolote kwa mashabiki wako?

Quick Rocka: Ninahitaji sapoti yao, bado nina safari ndefu sana kimuziki.

Chanzo: GPL

Comments

comments

Exit mobile version