Rais Magufuli Amfuta Kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dk. John Magufuli ametangaza kumfuta kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,Wilson Kabwe.
Hatua ya kumfuta kazi Mkurugenzi huyo imefuata baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kumwambia Rais Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, kuwa Mkurugenzi wa huyo wa Jiji alisaini mikataba kadhaa ambapo mmoja kati ya hiyo wa tozo za mabasi ya abiria ya kwenda mikoani imelisababishia taifa hasara ya shilingi takribani bilioni 3, ambapo kwa kila mwezi zilikuwa zinapotea shilingi milioni 42 tangu 2015- 2016.
“Jamani Mnataka mimi nifanyeje?, Mnataka nitumbue Jipu hapa hapa? Wangapi wanataka nitumbue? Basi kwa vile umezungumza wewe mkuu wa Mkoa, na mimi niliapa kusimamia sheria, na mimi viongozi wa namna hii hii ambao wanafaidi jasho la watu masikini kwenye Serikali yangu hawana Nafasi, Kwahiyo kuanzia sasa kabwe nime msimamisha kazi, Nendeni mkajulishe hivo, na hata ile miradi imesimamishwa kazi” Alisema Rais Magufuli.