Ni ukweli ambao waigizaji wengi wa filamu Tanzania wanaukataa, kwamba tangu Steven Kanumba afariki, kiwanda chao kimekuwa msege mnege!
Hakuna ushindani tena, hakuna excitement tena mtaani kama ilivyokuwa zamani kwenye tasnia hiyo. Mauzo ya filamu yameshuka, waigizaji wengi wamekata tamaa kitu kilichowafanya kufikiria Plan B ili kuendesha maisha yao.
Wasambazaji wa filamu nao wanadaiwa kupunguza idadi ya filamu wanazochukua na kuwafanya waigizaji wengi kubaki na kazi zao mkononi.
Lakini la msingi zaidi ni kuwa filamu zetu zimedumaa na kushindwa kupiga hatua ya mbele ya kujulikana kimataifa.
Haihitaji watu 10 kubadilisha mchezo mzima, bali mtu mmoja tu anaweza kutengeneza impact inayoweza kutumika kama chaji ya kuwapa nguvu wengine. Mungu alimchukua Steve Kanumba katika muda ambao nyota yake ilikuwa imeanza kung’aa kimataifa. Kanumba alikuwa ‘Diamond’ wa Bongo Movie.
Na sasa wakati ambapo inatubidi kukubali ukweli huo, kuna dalili za kumpata mtu anayeweza kukaribia caliber ya Kanumba, naye ni Rammy Galis.
Kwa watazamaji wa filamu ambao waliacha kufuatilia filamu za kibongo baada ya Kanumba kufariki, wanaweza wasiwe wanamjua muigizaji huyu. Wakati anaanza, wengi walimfananisha na Kanumba, kwa muonekano wake zaidi.
Na kwakweli ukimuangalia vyema, ni lazima atakukumbusha kuhusu Kanumba. Mimi nilimuona kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya Chausiku na nilipenda uigizaji wake – jamaa anajua sana. Galis ana potential ya kuja kuwa muigizaji mkubwa Afrika kama tu Tanzania ikiamua kumpa support.
Hivi sasa yupo nchini Nigeria, alikoenda kumalizia filamu yake mpya, Red Flag iliyoigizwa kwa kimombo tupu.
Rammy amepania kuipeleka bongo movie next level na kwakuwa ni msanii pekee mwenye ‘balls’ na ‘guts’ hizo, ni wajibu wetu kumuunga mkono na kumpa moyo. Kwenye filamu hiyo anaigiza na msanii wa kike wa Nollywood, Yvonne Jegede. Ni maarufu nchini Nigeria ambaye wengi watakuwa wanamfahamu kwasababu ndiye msichana anayeonekana kwenye video ya wimbo wa 2 Face, African Queen.
Muongozaji wa filamu hiyo kwa upande wa Nigeria ni mtu maarufu kwenye Nollywood ambaye Rammy anamuelezea kwenye video aliyopost Instagram; Napochukua Maagizo Ya Director Kijana wa #Nollywood Anayefanya Kazi Na Wasanii Wote wa Nchini Humu … #EtiSiNiKuombeaTu #MlangoEtiSiHuuApa.”
Pia amemtambulisha producer wa filamu hiyo kwa picha yake aliyoiandikia: Emmanuel Okwui Eneowo A.k.a Mr PERFECT himself .. One of the big producers in Nigeria Films , SHORTLY Atakuambia Kafanya kazi Ya Filamu na Nani Na Nani na Majina Ya Filamu Zake.” #Staytuned.
Naamini kuwa Rammy atafika mbali kwasababu kwa kujichanganya na watu muhimu kwenye Nollywood mapema, kutamsaidia kupata connection zaidi zitakazomsaidia kukuza jina lake.
Bolanle Ninalowo ni muigizaji anayedaiwa kuwa na uhusiano na Yvonne Jegede. Wote wataonekana kwenye Red Flag.
Nafurahi kuona kuwa tumeanza kupata watu wanaoweza kuthubutu kupambana kukuza filamu za Tanzania.
Kila lakheri Rammy.
Chanzo;Bongo5
Comments
comments