Rammy Galis na Rado Wametoleana Mapovu
WAIGIZAJI wawili kutoka Bongo Muvi, Rammy Galis pamoja na Rado wametoleana mapovu mazito huku Rado akisema kuwa Ramy kwake ni msanii mdogo sana.
“Kwanza Rammy amefanya filamu nje, hiyo sio Bongo Muvi hivyo mimi nafanya kitu halisia kutoka Tanzania na kingine Rammy ni msanii mdogo sana huwezi nishindanisha nae yeye ni viwango vya kina Gabo huko na akina Duma ila sio mimi,” alisema
Akijibu tuhuma hizo Rammy alisema kuwa kwake kafanya kitu tofauti na wala sio Bongo Muvi bali alichofanya ni kuivusha zaidi mbele Bongo Muvi.
“Unaweza kuwa mdogo lakini mkubwa kiakili, mimi ni mdogo kwa Bongo Muvi lakini nimefanya kitu bora sana hivyo si mbaya anachosema,” alisema Rammy.