Rapper wa Kike Chemical Adai Hajawahi Guswa na Mwanaume
Msanii wa kizazi kipya anaepeperusha bendera ya Tanzania kwa kupitia songi lake jipya linalokwenda kwa jina la “I’M SORRY MAMA” mwanadada Chemical, amesema yeye ni bikira(hakuwahi kujigi jigi tangu azaliwe).
Chemical ameongea hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha D’WIKEND CHATSHOW kinachorushwa kupitia clouds tv. Chemical ameongeza, licha ya kuwa bikira hajawahi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja(ulesbian).
Vilevile ameongezea, yeye hana gharama kabisa, kwasababu hatumii mavitu ya gharama kama wadada wa mjini(hapaki miwanja, haweki manywele ya bandia, na makororo mingine ya thamani) ambayo wadada wa mjini wamekuwa wakitumia.