NYOTA wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema kwa sasa amejikita katika kilimo cha matikiti maji na kupumzika kidogo katika uzalishaji wa filamu akiamini kuwa kilimo hicho cha matunda kinampatia maslahi zaidi kuliko filamu kwani hali ya soko ni tete.
“Mimi ni mtayarishaji mkubwa wa filamu, ninapoandaa kazi yangu ya sinema ni lazima nitumie pesa nyingi hivyo ni muhimu niangalie zinarudije. Nimejiongeza kwa kulima matunda kwani inalipa kwa sasa,” alisema Ray ambaye amenasa katika penzi zito la Chuchu Hans.
Ray alisema kuwa matunda ni sehemu ya chakula hivyo kila mtu anahitaji kula vinzuri na kupata matunda kwani suala la ulaji ni lazima si kitu cha anasa kama vitu vingine.
Alikwenda mbali na kudai kuwa filamu za Kitanzania zimekwama kutokana na soko kuvurugika hivyo kilimo huenda kikamtoa.
Mwanaspoti
Comments
comments