Artists News in Tanzania

RAY C Afungukia Kutoka na Mbunge

DAR ES SALAAM: Sexy lady mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi mbunge yoyote nchini kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakieneza ubuyu.

Rehema Chalamila ‘Ray C’

Ray C aliliambia Wikienda kuwa, mbali na kufahamiana na wabunge mbalimbali nchini, lakini hata siku moja hajawahi kujiingiza kwenye uhusiano na mheshimiwa yeyote kama inavyovumishwa.

“Kwanza kwa sasa mambo ya mapenzi nimeyaweka kando, niko bize na muziki wangu, akili na hisia zangu zote nimezielekezea kwenye kazi. Muziki ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Ray C.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Exit mobile version