Msanii wa kike aliyewahi kutikisa kupitia muziki wake kwa ufundi wa kukata viuno akiwa stejini mwanadada Ray C yuko mbioni kurudi tena kwenye game na tayari ameshafanya ngoma tano na zinatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
eNewz imezungumza na msemaji wa Wanene Entertainment Gentriez ambapo kwa sasa ndiyo sehemu ambayo Ray C anatengenezea ngoma zake na amefunguka kuhusu maendeleo ya Ray C kimuziki na kusema kuwa kwa sasa maendeleo yake ni mazuri sana na tayari wameweza kutengeneza nyimbo tano za msanii huyo.
“Maendeleo ni mazuri na sasa hivi Ray C tayari ameshatengeneza ngoma nne kama siyo tano ambazo tayari zimekamilika tunasubiri tu ziingie sokoni , baada ya Songa atafata Damian Soul halafu ndio atafuata Ray C”
Wanene Entertainment wameweza kumsaini Damian Soul na wamesema kuwa bado kuna wasanii wengine watafuata akiwemo msanii kutoka Kenya ambapo wamedai kuwa bado wako kwenye mazungumzo.
eatv.tv
Comments
comments