Ray Kufungua Mwaka na ‘Tajiri Mfupi’
Staa mkali wa Bongo Movies, Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye pia ni moja kati ya wakurugezi wa kampuni ya utengenezaji wa filamu ya RJ anatarajia kufungua mwaka huu wa 2016 kwa kuuachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la Tajiri Mfupi ikiwa imesheheni mastaa wakali kama Ray mwenyewe, Muhogo Mchungu, Batuli na wengineo.
Akiongea na chanzo cha habari hii, Ray ambaye yupo kwenye harakati za kuifanyia ‘promo’ kazi yake hii itakayoingia sokoni mwezi wa pili mwaka huu, alieleza kuwa hii ni moja kati ya kazi zake bora kabsisa tangu aanze kuigiza.
Kuwa wa kwanza kuiona Trailer ya filamu hiyo hapa.