MWIGIZAJI Muongozaji na mtayarishaji wa filamu Vincent Kigosi Ray ameteka kila kona ni yeye kuliko hata game ya Yanga na samba wala watu hawana habari na matokeo ya kidato cha nne kila mtu ni Ray Ray, hiyo inaonyesha msanii huyo ni Nyota kweli katika tasnia ya filamu Bongo.
Huku akijiandaa kuachia filamu yake ya Tajiri mfupi kila anapoposti ujumbe wowote unakiki na kuwa habari ya mjini na kufunika mambo muhimu katika jamii jambo ambalo wachambuzi wa mambo wanasema kuwa msanii huyo anakubalika sana katika jamii na anafuatiliwa kwa ukaribu.
“Mimi kwa sasa sitaki ustaa ambao watu wanalilia kwani nilishupta kitambo tumekwenda DRC Congo watu wamekufa kwa ajili ya kumuona Ray the Greatest ndio maana kwa sasa nimejikita katika kazi nikiposti kitu cha kawaida kabisa inakuwa dili kwa wengine,”anasema Ray
Ray anasema kuwa anawaomba wapenzi wa filamu wajiandaa kuipokea filamu ayke kali nay a kusisimua ya Tajir Mfupi kwani amefanya maajabu makubwa hayajawahi kutokea katika tasnia ya filamu Bongo anaamini kabisa kwa upepo aliouona ni wazi kazi yake itakuwa tishio.
“Kama vile watu mnavyokuwa wabunifu katika kuposti habari zangu basi nawaomba nguvu hizo zipelekeni katika kununua filamu yangu ya Tajiri mfupi ili niendelee kuwapa vitu adimu na vizuri tupo pamoja mwezi tajiri mfupi inaingia sokoni ikisambazwa na Steps Entertainment,”
Comments
comments