Artists News in Tanzania

Raymond Atuhumiwa Kuiba Mistari Kwenye Wimbo wa Msanii wa Singeli

Msanii wa WCB, Raymond anatuhumiwa kutumia baadhi ya mistari ya wimbo wa msanii wa muziki wa Singeli, Manyo Lee kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sugu’.

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Manyo Lee amesema, “Mimi nilisikia kwa watu tu kuwa dogo kachukuwa mashairi yangu. Juzi kati lilifanyika tamasha kubwa tu nikaona akiimba yale mashairi lakini nikaona kawaida tu lakini hivi karibuni nimeona kaachia video kabisa nikaona kumbe dogo yupo serious kabisa.”

“Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu funga virago shetani. Joh Makini akiwa mweusi Barakah tumuite nani?,” mistari ambayo Raymond anadaiwa kuchukua kwenye wimbo wa msanii huyo unaoitwa ‘Mwendo wa Pushapu’.

Naye Manyo Lee katika wimbo wake aliouachia mwezi Septemba mwaka huu ameimba, “Kama pochi ya dada naiminya kwapani, namuamini Mungu virago funga shetani. Makini ajiite mweusi na Nigga ajiite nani?.”

Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version