Richie Awapa Neno Wapiga Picha za Utupu
Msanii wa filamu za kibongo Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie, ametoa sababu ya wasichana wengi sasa hivi kukimbilia kufanya ‘video vixen’ ambako hutumia kama kivuli cha kufanya mambo machafu, tofauti na kipindi ambacho wao walianza sanaa.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio walipokuwa wanatambulisha kipindi chao kipya cha ‘Barazani’, Richie amesema kwamba mabinti wa sasa wanafanya hivyo kwa kujitafutia pesa, lakini anashangazwa na yale wanayoyafanya zaidi ya video vixen, ikiwemo kupiga picha za utupu.
“Mabinti wengi kuingia huko ni kwa lengo la kutafuta kupenya, kwa mtazamo wangu umri wao unaruhusu na hiki kipindi kilichopo, lakini sio sahihi kukimbilia huko kwa umri mdogo walio nao, kwani kuna mambo mengi ya kuyafanya ili waendeleee, sijui wamekimbilia nini huko”,alisema Richie.
Hivi karibuni msanii huyo akiwa na wenzake wanatarajia kuzindua kipindi chao cha Brazani kitakachorushwa na East Africa Television, ambacho kitakuwa kinasimamia mfumo wa kazi zao na usambazwaji wa kazi za sanaa.
Chanzo:GPL