MWIGIZAJI wa kike mwenye jina kubwa na nyota Swahilihood Riyama Ali amefunguka kwa kusema kuwa mwaka huu umeingia kwake akiwa na majonzi baada ya kumpoteza baba yake mzazi Mzee Ali aliyefariki wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam na kuzikwa huku Mjimwema Kigamboni.
“Siku zote mandhila hayazoeleki hata huwe jasiri vipi unapompoteza mzazi lazima unaishiwa na nguvu nimempoteza baba yangu aliyefariki hivi karibuni na kuanza mwaka kwa huzuni, lakini kila jambo inatupasa kushukru kwa Mola wetu,”alisema Riyama.
Mwigizaji huyu asiyechuja katika uigizaji kwa miaka mingi amesema kuwa mwaka huu mpya anatarajia kupaa zaidi na si kushuka kwani yeye kinachomsaidia anajua miiko ya sanaa jambo ambalo linamfanya azidi kung’ara kwani filamu kwake ni kazi ya maisha yake hauifanyii masihara kabisa.
Filamu Central
Comments
comments