Riyama Ally Amefungukia Maumivu Aliyoyapata Alipopoteza Mtoto
Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally aelezea maumivu aliyoyapata kipindi alichopoteza mtoto.
Akizungumza na gazeti la mwanaspoti, Riyama anafichua kuwa mwaka 2000 aliwahi kupata mtoto akafariki, baada ya hapo alikuwa anatamani kubakia mpweke siku zote kwa sababu ya simanzi aliyopata.
“Maumivu niliyosikia kwa kumpoteza mtoto wangu yule, ilinifanya nitamani kuwa mpweke tu, lakini kwa vile nilipokuwa mdogo nilibahatika kupitia madrasa na kufundishwa masuala ya kiimani, nilimshukuru Mungu na kumuachia yeye kwa kuamini kuwa kazi yake haina makosa,” anasema.
Riyama aliongeza kuwa anasema kabla hajaingia kwenye uigizaji alikuwa mfanyabiashara mzuri wa kukopesha vitu mbalimbali vya majumbani ila yeye alikuwa tofauti na wenzake, kwani hakuwahi kula mtaji kwa sababu alikuwa mjanja na mbabe vile vile.