Artists News in Tanzania

Riyama,Muhogo, Bi. Hindu na King Majuto watajwa kwa umahiri wa Kiswahili!

BODI ya ukaguzi na filamu na michezo ya kuigiza ilifanya warsha kwa wasanii wa filamu Jiji la Mwanza kwa mafanikio makubwa sana kwa kupata wasanii washiriki wengi ambao wamepata elimu kutoka kwa wawezeshaji mahiri katika masuala ya filamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na Dodoma.

muhogo

Muhogo Mchungu

Akiongea na FC Katibu mtendaji wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo amesema kuwa serikali imejipanga kujenga weledi kwa wadau wa filamu nchini kwa sababu wamekuwa wakikutana na sinema zenye matatizo mbalimbali hivyo baada utafiti wameanzisha program ya mafunzo.

Semina hiyo kwa Jiji la Mwanza ni ya pili kufanyika baada ya warsha ya kwanza kufanyika mkoani Morogoro huku wasanii wakijitokeza kwa wengi na kufurahia semina hiyo ambayo ni mpango kazi kwa Bodi ya filamu kuwajengea uwezo wasanii kuleta ushindani kwa Afrika Mashariki.

Riyama Ally

“Pamoja na kuwa tunazalisha filamu nyingi kuna changamoto zake kuhusu sinema nyingi kutawaliwa na maudhui ya kimapenzi na kuacha vivutio vingi kama vile mbuga za wanyama na sehemu nyinginezo,” Bi. Fissoo.

Kulikuwa na mada ambazo zimewafungua wasanii huku moja ya matatizo yanayowakabili hasa wasanii wakubwa ambao wamepoteza nafasi za mialiko sehemu maalum au kukosa matangazo ya biashara akiongelea hilo Ndugu Innocent Mungi kutoka meneja mawasiliano Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) .

Matumizi mabaya kwa wasanii
Mwezeshaji huyo amedai kuwa wasanii wengi wameshindwa kutumia mitandao vema na kujikuta wakipoteza nafasi za biashara kutokana na mitandao akasema kuwa kwa wasanii wanaotengeneza fedha kwa kutumia mitandao ni wawili tu Emmanul Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ na Nassib Abdul ‘Diamond’

“Wasanii wameshindwa kutumia mitandao ya kijamii katika kujipatia fedha na badala yake wanatumia mitandao katika kujidhalilisha kwa kuposti picha zisizo na maadili, lakini kama wanaweza kuwa makini wana njia nyingine ya kutengeneza fedha,”alisema Mungi.

Mzee Majuto

Lugha ya Kiswahili ni mtaji mkubwa ambao pengine watengenezaji wa filamu wameshindwa kuutumia kutokana na matumizi ya kuchanganya lugha za kigeni japo si kwa umahiri mkubwa na kubaisha kuwa wasanii wanaotumia Kiswahili vizuri ni Abdalah Mkumbila ‘Muhogo mchungu’, Bi. Hindu, King Majuto na Riyama Ally.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa Lugha kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni , Michezo na Sanaa Hajat Shani Kitogo akiwakilisha mada iliyosema Filamu katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kimataifa akisema kuwa akiwa Zanzibar katika kongamano la CHAWAKAMA .

Wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda walidai kuwa wamekuwa wakifaulu mitihani yao ya Lugha ya Kiswahili kwa kujibu maswali kwa kutumia sinema zinazoigizwa na King Majuto, Riyama, Bi. Hindu Muhogo Mchungu.

Kufuatia mafunzo hayo kufanikiwa mmoja ya wasanii na mwalim Mkongwe katika tasnia ya ufundishaji ndugu Fumbuki Lubasa alipotoa zawadi ya kiwanja cha kujenga Studio kubwa ya uzalishaji wa filamu na vipindi.

Kiwanja hicho kipo maeneo ya Nyegezi chenye ukubwa wa 50 kwa 40, Mwl. Lubasa alitoa kiwanja hicho kwa ajili ya hali halisi inayowakumba wasanii wengi nchini kukosa mitaji na sifa za kukopesheka hivyo watumie eneo hilo ambapo mfuko wa jamii wa PPF umeahidi kulifanyia kazi hilo kwa ajili ya kuangalia kama inaweza kuwekeza.

Bi Hindu

Mafunzo hayo ya siku tatu yalifunguliwa na Katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Mwl. Hamis Maulid na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Tesha Onesmo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, mkuu wa Wilaya alifurahia sana mafanikio ya semina hiyo na kusema.

“Jamani niwapongeze sana Bodi ya filamu kwa kutuletea warsha hii iliyozaa mafanikio makubwa kwa wanamwanza Ujanja kuwahi sasa watu wa Dar es Salaam wajipange tutafanya makubwa katika filamu, lazima Mwanza iwe nambari moja katika filamu,”alisema Mh. Tesha.

Filamu Central

Comments

comments

Exit mobile version