RJ Mbioni Kudondosha ‘Tajiri Mfupi’-Ray
Muigizaji mkongwe na mkurugenzi wa kampuni ya RJ inayojihusisha na utengenezaji wa filamu hapa bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amedokeza kuwa kwa sasa kampuni hiyo ipo mbiyoni kuachika filamu yao mpya inayokwenda kwa jina la TAJIRI MFUPI.
‘Kampuni yako ya kizalendo nchini Tanzania RJ company (Best Quality Ever!) ipo mbioni kudondosha mzigo wa kufa mtu ‘Tajiri Mfupi’ wapo wasanii wakali kibao yupo Grace Mapunda ,Yobinesh (Batuli)Abdalah Mkumbila (Muhogo Mchungu)Idrisa Makupa (Kupa) na wengine wengi lini inatoka? tega sikio lako na macho yako.”-Ray aliandika hayo kwenye ukurasa wake mtandaoni.
Jionee Trailer lake hapo jini.