Msanii wa filamu nchini,Rose Ndauka ameitaka serikali kuongeza nguvu katika kusimamia kazi za wasanii.
Rose ametoa kauli hiyo alipokuwa akiuzungumzia utendaji wa Rais Magufuli katika kipindi cha mwaka mmoja toka achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kwenye tasnia ya filamu nikimuongelea Rais John Pombe Magufuli mi mabadiliko ninayoyafikiria ni mabadiliko zaidi ya haya ambayo tupo nayo sasa hivi. Mwaka mmoja wa Rais Magufuli serikali kuweza kusimamia kazi zetu vizuri, kuwe na muongozo mzuri kwenye upande wasanaa ili na wale producers au wale distributors waweze kujua kabisa sheria ziwe wazi,”Rose aliiambia TBC.
Rais Magufuli ametimiza mwaka mmoja tangu aingine madarakani hivyo watu mbalimbali wamekuwa wakiuzungumzia utendaji kazi wake.
BY: EMMY MWAIPOPO
Comments
comments