Artists News in Tanzania

Rose Ndauka: Filamu Bongo Hazijashuka

Staa wa Bongo Movie, Rose Ndauka amedai kuwa ni upepo mchafu umepitia soko la filamu nchini na si kama ni kweli filamu zimeshuka thamani kama watu wanavyodai.

Muigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa baadhi ya wasanii wanazidi kujitahidi kufanya vizuri lakini kilichopo kwa sasa ni upepo mchafu umepitia tu.

“Huu ni upepo mchafu umepita lakini wasanii wanajitahidi sana kufanya filamu nzuri. Tumeweza kuona wakina Wema Sepetu wameenda mpaka Ghana kufanya movie na wasanii wa nje. Soko la filamu halijashuka kwa kuwa bado mashabiki wanaendelea kufuatilia na kusupport,” amesema Ndauka.

Rose ameongeza mashabiki watarajie filamu nyingine mwakani kutoka kwa wasanii wa ‘Ndauka Family’ kwa sasa waendelee kufurahia filamu ya ‘Angela’ iliyotoka mwezi Mei, mwaka huu.

Bongo5

Comments

comments

Exit mobile version