Rose Ndauka Kuwa Mtangazaji wa Runinga
Malkia wa filamu, Rose Ndauka atakuwa mtangazaji wa kipindi kipya cha runinga kiitwacho ‘SK TV Show’.
Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, atakuwa akitangaza kipindi hicho cha runinga akiwa na Fahad Fuad.
SK TV Show ni kipindi ambacho kitakuwa kinatoa habari mbalimbali pamoja na matukio yanayotokea katika jamii.
Hata hivyo mwigizaji huyo hakuweka wazi kipindi hicho kitaanza kuonekana katika runinga gani.
Bongo5