Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally aliyetobolewa macho maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
Makonda ametoa majibu hayo ofisini kwake Ijumaa hii.
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote,” alisema Makonda.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake,” alisema.
Pia Makonda amesema serikali itatoa kiasi cha shilingi milioni kumi kama sehemu ya mtaji wake. “Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja,” aliongeza.
Kupitia Instagram pia, Makonda ameandika: Watanzania wengi tulitamani Said uone tena ila tumeshindwa, tuna mwachia Mungu.
Tayari mtu aliyemfanyia Ukatili huo yupo mahabusu.
BY: EMMY MWAIPOPO
Comments
comments