Msanii mkongwe wa vichekesho nchini maarufu kwa jina la Senga, amepiga stori na eNewz na kufunguka kuhusu sanaa ya vichekesho nchini na kusema kuwa Bongo kwa sasa wachekeshaji ni wachache sana, na kwamba wengi ni waigizaji.
Senga alisema wengi wanaojita wachekeshaji kwa sasa ni watu ambao si comedians, bali ni waigizaji wa kawaida wanaolazimisha tu kuchekesha.
Senga alishauri akisema “Wachekeshaji wanapaswa kujifunza kutumia vitendo zaidi katika maigizo yao ili kazi zao ziwe za kimataifa”.
Senga alimalizia kwa kusema kiswahili ni lugha inayoeleweka nchi chache tu, hasa Tanzania hivyo kutumia maneno mengi kwenye ucheshi ni kujifungia milango ya kupata soko la kimataifa.
Comments
comments