-->

Serikali Kuandaa Sera Itakayosaidia Sheria ya Filamu

Dar es salaam.Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema itaanza kukusanya ya wadau wa filamu ili kuandaa sera itakayosaidia kutengeneza sheria mpya itakayosimamia tasnia hiyo kulingana na mazingira ya sasa.

Zoezi la ukusanyaji wa maoni litahusisha makundi mbalimbali wakiwemo watayarishaji, waigizaji na wasambazaji wa filamu.

Akizungumza kwenye kikao cha kujadili changamoto na mwelekeo wa tasnia hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema makundi yote yanapaswa kujitokeza kutoa maoni kulingana na changamoto wanazokabiliana nazo.

“Lazima tukubali wasanii mnatumia nguvu kubwa kufanya kazi lakini hamnufaiki, hamtakiwi kurudi nyuma. Tasnia hii ina sheria ya kipuuzi lazima tuanze mapema kujadiliana ili baadaye tutoke na mwongozo mzuri.”

By Fredrick Nwaka, Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364