SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake.
Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.
Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam.
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa kumwona walimweleza shida yao na kuanza kazi ya uchunguzi ili kutafuta dawa za kulevya.
Aliongeza kwamba baada ya hapo walifanya uchunguzi ndani ya chumba cha wafanyakazi wa ndani wa kike, walikuta msokoto wa bangi uliotumika ndani ya kibiriti na baadaye walijaza hati ya ukamataji, kisha kuondoka na Wema hadi kituo cha polisi.
Aidha shahidi huyo aliiomba mahakama ipokee kielelezo hicho mbele ya Mahakama ambapo wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alipinga kupokelewa kwa hati hiyo, akidai ina mapungufu ya kisheria.
Kutokana na mvutano huo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kutoà uamuzi wa kupokea kielelezo hicho ama la.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
comments