Shamsa Achekelea Mpenzi Mpya
STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha furaha yake ya kuumaliza mwaka kwa kumpata mpenzi mpya, ambaye hata hivyo, alikataa kutaja jina lake.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Shamsa alisema mwaka huu pia umeweka historia kwa yeye kuweza kutimiza mambo yote aliyojipangia tangu alipoachana na baba wa mtoto wake.
“Nafurahi sana namaliza mwaka nikiwa nimetimiza malengo pia kuwa na mpenzi mpya ambaye ni mume wangu mtarajiwa, ndani ya mwaka huu nimejifunza siyo vizuri kuweka uhusiano wazi hasa kwenye mitandao ya kijamii, maana unajidhalilisha unaweza kujikuta leo uko na huyu kesho na huyu inakuwa ni aibu,” alisema Shamsa.
Chanzo:GPL