Shamsa Amfungukia Haya Gabo Zigamba
Msanii Shamsa Ford ameweka wazi hisia za moyo wake kwa Gabo Zigamba kuwa ndiyo mwanaume pekee anayemkubali pindi wanapokuwa pamoja katika kazi za filamu na kuhisi kila wanachokifanya ni ukweli na uhalisia.
Shamsa amebainisha hayo kupitia moja ya mtandao kijamii anaoumiliki kwa kuweka picha inayowaonesha wawili hao wakiwa mbali kihisia huku ikiwa imebebwa na ujumbe mzito ambao ulisababisha baadhi ya mashabiki zake ‘kutokwa na povu’.
“Kiukweli ni mwanaume pekee ambaye nikiigiza naye huwa nasahau kama ninaigiza na kuhisi ni kweli..namkubali sana huyu mmakonde wangu…Gabo Zigamba ‘On SET'”. Ameandika Shamsa Ford
Aidha mashabiki zake walimkosoa kitendo hicho kwa kumuomba ajitambue kuwa yeye sasa ni mke wa mtu na anapaswa kuangalia kila anachofanya kisije kuzidi mipaka yake, huku mwingine aliandika kwa kumuuliza hayo maneno endapo mume wake Chid mapenz akiyaona itakuaje.
Hii ndiyo post yenyewe…..