Shamsa Ford Aeleza Jinsi Ndoa Ilivyobadili Maisha Yake
Malkia wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kuzungumzia jinsi ndoa ilivyobadili maisha yake.
Mwigizaji huyo miezi miwili iliyopita alifunga ndoa na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.
Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Shamsa amesema ndoa imempatia amani ya moyo ambayo alikuwa anaitafuta kwa muda mrefu.
“Namshukuru mwenyezi Mungu kwa afya njema na kwa kila kitu, kikubwa ndoa imebadilisha vitu vingi sana katika maisha yangu, kwanza imenifanya kuwa mwanamke kamili, mwanamke wa kitanzania heshima kubwa ni ndoa. Lakini pia ndoa imenifanya niache baadhi ya vitu na kuongeza baadhi ya vitu katika maisha yangu,” alisema Shamsa.
Aliongeza, “Kiufupi maisha yangu yamebadilika sana, sasa hivi kuna vitu ambavyo siwezi kuvifanya tena, kwa sababu chochote nachokifanya lazima niombe ruhusa yake. Pia nimekuwa na amani na furaha ambayo naipata kwa mume wangu, na sasa hivi na-enjoy maisha nafuraha ambayo nilikuwa sina mara ya kwanza, kwa hiyo nikitendo ambacho namshukuru sana mwenyezi mungu,”
Pia mwigizaji huyo amewataka mashabiki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa filamu zake mpya.
Bongo5