Shamsa Ford Awatolea Uvivu Wasioolewa
Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amefunguka na kuwachana baadhi ya wasanii wa kike na watu maarufu ambao hawataki kuolewa au wanasubiri waje kuolewa na watu wenye fedha zao na kudai kuwa watasubiri sana mpaka sura zao ziote sugu.
Shamsa Ford amesema hayo wakati akimpongeza msanii Shilole baada ya kuolewa
“Hongera sana mamy. Umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.Cha muhimu uwe mke bora wa kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni. Mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana Inshaallah mtazikana. Karibu kwenye Chama mama” aliandika Shamsa Ford
Aidha Shamsa Ford hakuwaacha salama wale wadada na wasanii ambao wamekuwa hawataki kuolewa na watu wa kawaida
“Sasa nyie mnao subili matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubili sana mpaka uso uote sugu. Uzuri na Ustar una mwisho wake, itafika muda hata inzi hakusogelei” alisema Shamsa Ford