Shamsa Ford: Baada ya Posa Muda Wowote Naolewa
BAADA ya kutolewa barua ya uchumba na mpenzi wake mpya, Chidi Mapenzi, mwigizaji, Shamsa Ford, amefunguka kwamba wakati wowote atafunga ndoa na mwanaume huyo kwa kuwa mipango yao imeshakamilika.
Shamsa aliliambia MTANZANIA kwamba licha ya kupitia katika changamoto za wapenzi wengi, mpenzi wake huyo wa sasa ndiye aliyeonyesha ushawishi hadi kutaka kumuoa.
“Kwa hatua hii najivunia, hadi mwanaume akushawishi muoane huyo ana nia njema na heshima kwangu,” alisema Shamsa.
Pia Shamsa aliwaeleza wapenzi wa filamu zake kwamba wataendelea kupata burudani zake hata kipindi atakachokuwa ameolewa.
Mtanzania