Shamsa: Nilijua Matatizo yatamkuta mume wangu!
SIKU chache baada ya mumewe, Chid Mapenzi kupata msala wa madawa ya kulevya na kuswekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro), Muigizaji Shamsa Ford amesema kamwe haiwezi kutokea akamuacha mumewe kwani tangu awali, alijua siku moja mumewe anaweza kupata matatizo kama hayo.
Muigizaji huyo alisema tayari mitandaoni kumeshaanza kuenea uvumi kuwa huenda akamuacha mumewe kutokana na matatizo aliyoyapata jambo ambalo kamwe hawezi kulifanya kwani alipoingia kwenye ndoa, alijua atakutana na changamoto nyingi ikiwemo hiyo ya mumewe kulazwa polisi.
“Nilifahamu tangu naingia kwenye ndoa kwamba nitakutana na changamoto kama hizi. Nilijua siku moja mume wangu anaweza kupata matatizo hivyo kamwe siwezi kumtenga kwa namna yoyote ile,” alisema Shamsa. Hadi sasa, mumewe huyo bado anashikiliwa na polisi ambapo upelelezi ukikamilika atafi kishwa mahakamani.
Chanzo:GPL