Shela la Aunt Lazua Maswali Tata
KUNASWA kwa msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa ndani ya gauni la harusi (shela) kumezua maswali tata huku wadau wakiamini alikuwa safarini kwenda ukumbini kwa ajili ya harusi yake.
Aunt alinaswa hivi karibuni akitoka ndani ya saluni moja iitwayo Wedding Dover, Sinza Afrikasana akitoka akiwa ndani ya shela hilo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya watu waliamini Aunt alikuwa kwa ajili ya sherehe hizo kwani kuingia kwake saluni hapo mpaka kutoka akiwa amepambwa kulichukua saa moja.
“Hizo picha mimi nimezipata akiwa ndani ya hoteli maarufu pale Sinza Afrikasana. Kila mtu alisema bibiye kafunga ndoa kwa siri na mzazi mwenzake, Iyobo (Moses) na harusi yake ni kwa siri,” kilisema chanzo.
Baada ya mwandishi kunasa habari hizo, alimtafuta Aunt ili aweze kuzungumzia kuhusu kuvaa gauni hilo ambapo alichenga na kusema kuwa muda utakapofika ataweka wazi kila kitu.
“Unajua kila mtu katika maisha yake na taratibu zake, sasa mimi bado sijapanga kulizungumzia hilo la kufunga ndoa ya siri mimi na Iyobo. Ila muda ukifika nitaweka wazi kila kitu. Hilo gauni lisikutishe ndugu yangu,” alisema Aunt.
Chanzo: GPL