Msanii wa bongo fleva, Shetta amefunguka leo kuhusiana na taarifa zilizozagaa kuwa mkewe, mama Qaila kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond.
Akiongea na cloudsfm, Shetta ameeleza haya;
‘’Nilifuta picha zote kutokana na ‘management’ yangu katika hali ya kunitengeneza Shetta mpya unajua kila mwaka unatakiwa kuwa mpya kwa kila kitu, sasa hivi nina timu mpya ya watu kwenye ‘management’ yangu kwahiyo mmoja wa meneja wangu akaniambia kwa mtazamo naona udelete picha zote tuanze na kitu kipya kwahiyo nikafuta picha zote na watu wanaona katika kuanza nimeanza na logo kwenye akaunti zangu za kwenye mitandao hiyo ilikuwa ni process ambayo tulikuwa tumeianza,kwahiyo suala la kufuta picha halihusiana na ishu yoyote ni suala la ‘management’ yangu tu na kumtengeneza Shetta mwingine’’ Alisema Shetta.
Akaendelea;
‘’Lakini pia ile skendo ya Diamond na mke wangu mama Qaila nafikiri ni ukaribu wangu na Diamond watu wanapenda kukuza vitu kama ambavyo imeanzia kwenye picha, na Diamond na suala la mama Qaila halipo sahihi kabisa na walioikuza hii ishi ni hizi timu za kwenye mitandao ‘sometimes’ mimi na Diamond huwa tunajiuliza au pengine kutokana na ukaribu wetu au watu hawapendi’’
cloudsfm.com
Comments
comments