Shilole amempongeza Nuh Mziwanda kwa kuongeza idadi ya wasanii walioukimbia ukapera baada ya kufunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake Nawal.
Kupitia mtandao wa Instagram, Shilole ameandika ujumbe unaosomeka, “Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie baraka tele kwenye ndoa yenu.”
Hitmaker huyo ameungana na mastaa wengine waliofunga ndoa mwaka huu akiwemo Mwana FA, Shamsa Ford, Nyandu Tozzy, Tunda Man, Mabeste na wengine.
Nuh na Shilole waliwahi kuwa wapenzi kwa muda mrefu lakini mwishoni mwa mwaka jana waliachana huku kila mmoja akianzisha mahusiano mapya.
Bongo5
Comments
comments