Shilole Atoboa Siri ya Kuolewa Kimya Kimya
Shilole alitoa ahadi kuwa atafunga ndoa kabla ya mwaka huu kuisha na kuwahaidi mashabiki wake kuwa atawatangazia siku ya ndoa yake lakini hakutekeleza ahadi yake hiyo na badala yake mashabiki wake waliona tu picha zake akiwa tayari amefunga ndoa.
“Mimi tayari nimeshafunga ndoa kama mlivyoona picha lakini naomba mashabiki zangu msijali ndoa tayari lakini kutakuwa na sherehe kati ya tarehe 20 au 25 mwaka huu kwahiyo mashabiki wangu mjiandae kula na kusaza mpaka vyakula vingine mtaondoka navyo,”amesema Shilole
Siku chache zilizopita Shilole alifunga ndoa na mpenzi wake Uchebe na kesho yake picha kusambaa mitandaoni
EATV.TV