Msanii Dogo Janja ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Kidebe’ na kuwa gumzo mtaani kutokana na kuwasifia baadhi ya wasanii huku wengine akiwaponda, ambapo ndani yake amemtaja mtu anayeitwa ‘Siwema’.
Dogo janja ametoa ngoma hiyo wakati wimbo wake wa ‘My Life’ ukiwa badi ni miongoni mwa ngoma ambazo mashabiki wengi wanazikubali huku wengi wao awali wakidhani kuwa asingeweza kufanya wimbo mwingine zaidi ya huo,
eNewz ilitaka kufahamu kuhusiana na chanzo cha Dogo janja kumsema Siwema ambaye anajulikana alikuwa ni mpenzi wa rapa Nay Wa Mitego na kubahatika kuzaa naye mototo mmoja kwa kusema “Siyo kiburi siyo mchafu kama Siwema” katika ngoma hiyo.
Dogo Janja aliamua kujitetea kuwa Siwema aliyemtaja katika ngoma hiyo siyo Siwema wa Nay wa Mitego bali ni msichana mwingine kutoka Arusha mtaa wa Ngarenaro.
Pia alifafanua zaidi kuwa wapo wengi wanaoitwa Dogo Janja lakini sio Dogo janja yeye.
“Mimi sijamzungumzia Siwema wa Nay wa Mitego, Siwema pale mtaani kwetu Ngarenaro kuna mwanamke anaitwa Siwema anatabia za kimiyeyusho yaani siyo mchoyo watu wengi wanapaa sana” Alisema Dogo Janja kufafanua mstari wake.
eatv.tv
Comments
comments