Artists News in Tanzania

Sijawahi na Sitokuwa na Mpenzi Mcongo -Wema Sepetu

Muigizaji mwenye umaarufu mkubwa kwenye filamu za kibongo Wema Sepetu, amemkana raia wa Kongo ambaye watu wengi wanadai ana mahusiano naye ya kimapenzi.

Katika ukurasa wake wa instagram Wema Sepetu ameandika juu ya taarifa hiyo na kusema kuwa hana mahusiano na raia huyo mkongo anayejulikana kwa jina la Apocalypse, sipokuwa anamfahamu kama rafiki tu kwake.

“Sijawahi na sitowahi kuwa na mwanaume Mcongo wa aina yoyote ile, sasa nashangaa watu wameona mimi ndo daraja la kuwapa umaarufu, I’m tired, huyo Apocalypse sijui kitu gani aint my man, I only know him as a friend, So please guys…. Niacheni kidogo tafadhal… Alam-siq…!!”, aliandika Wema Sepetu.

Pamoja na hayo Wema Sepetu amesema iwapo mtu huyo angekuwa na mahusiano nae angeweka wazi, hivyo watu waache kumpa kiki mtu huyo ambaye anadai kutafuta umarufu kupitia kwake.

“And ontop of all that I think u all know me by now nikiwa na mtu sijivungi kumtangaza maana huwa I live to please my heart…

Mwanaume wangu nadhani anajulikana… Sasa endeleeni kumpa huyo baba attention sababu yeye nako naona kashaona ni kamchezo kakupatia followers… Na nyie mnampa airtime ya kutosha…. So anaendelea… Ananiudhi na mimi kiukweli hadi napata hasira… But nakaa tu kimya”, aliandika Wema Sepetu.

Comments

comments

Exit mobile version