Sina Mpango wa Kumtafuta Said Fella -Juma Nature
Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Juma Nature, amesema hawezi kumfuata bosi wake wa zamani Said Fella kumtaka afanye nae kazi tena kama zamani.
Nature maarufu kama kiroboto ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha E News kinachorushwa na EATV na kusisitiza kuwa kama hajafuatwa yeye hawezi kwenda kumuomba afanye naye kazi.
”Mimi siwezi kwenda kumuomba Fella nifanye naye kazi ila kama yeye ananitaka kibiashara aje tukae chini tuandikishane mkataba unaoeleweka hapo sawa lakini hivi hivi sina mpango wa kwenda kwake, maana najiamini na mambo yanakwenda vizuri”Amesema Juma Nature.
Msanii huyo kwa sasa anarekodi video mpya na msanii Shetta na kuongeza kuwa video hiyo ikitoka itakuwa habari ya mjini kwa namna ambavyo ameipangilia na mashairi yaliyo ndani yake.
Aidha kwa sasa Said Fella ni Diwani wa kata ya Kilungule jijini Dar es salaam na pia ni meneja wa Yamoto bendi na TMK wanaume family.
Eatv.tv