Sipendi kuisikia ‘DSM Stand Up’ – Chid Benz
Msanii Chid Benz amesema huwa hapendi kuisikiliza nyimbo yake ya Dar es salaam Stand Up na kwamba hata anapo ‘perform’ jukwaani hujisikia vibaya.
Chid Benz ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema ukubwa wa wimbo huo unamuumiza hisia zake, hivyo hujisikia vibaya kila anapousikiliza.
“Hii nyimbo sipendi kuisikiliza kwa sababu inaniumiza ni ngoma kubwa flan kubwa sana, hata nikiwa na perform ile watu wanashangilia , kelele nini ndiyo inanipa ushindi ila inanipa hisia tofauti”, alisema Chid Benz.
Chid Benzi amesema ngoma hiyo aliiachia kwa baraka za mama yake, baada ya kumuambia aitoe kwani ndiyo ilikuwa ngoma bora kati ya nyimbo 80 alizokuwa amerekodi kabla haijatoka.
“Dar es slaam stand up ilikuwa ndani ya nyimbo hizo 80 nilizorekodi, siku moja mama yangu akaniambia ule wimbo unaoanza unalia tttt uko wapi? nikamwambia, ngoja nikutafutie, akaniambia hii itoe, nzuri hii nikaichukua nikaipeleka kwa Duly nikamkuta Pancho, nikamuita Ditto akaja kuweka sauti na tukaifanyia kazi”, alisimulia Chid Benz.
eatv.tv