Artists News in Tanzania

Sitaki ‘Collabo’ na Wasanii wa Bongo – Q Chillah

Msanii wa bongo fleva Q Chila amesema hakufanya kolabo na wasanii waliosainiwa kwenye lebo moja ya QS kwa sababu hakwenda pale kwa sababu ya kufanya kolabo na wasanii hao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Nay, H_Baba na wengine.

Akiongea kupitia eNewz Q Chila amesema kwa sasa anafanya kolabo na wasanii wa nje zaidi ili kuweza kutambulika kimataifa zaidi na hasa kwa nchi za Afrika kwa kuwa hapa Tanzania hata akifanya kolabo na wasanii wa hapa ataambiwa anabebwa kimuziki.

Hata hivyo Chillah alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa ana mpango wa kufanya kolabo na msanii  nguli wa bongo fleva Solo kwa kuwa yupo Tanzania na ni mtu anayeamini kwamba wakifanya kolabo la pamoja litakuwa poa sana.

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version