Sitaki Kuteseka Miye – Rose Ndauka
ROSE Ndauka muigizaji wa filamu Bongo anasema kuwa maisha yana nafasi kubwa kwa mwanadamu na unaposhindwa kufanya hivyo lolote linaweza kutokea, endapo kuna jambo unalifanya kama ni sehemu ya kujitatua kimaisha na ugumu kutokea ni kubadilika na kuangalia njia nyingine itakayokusaidia.
“Maisha yana nafasi nyingi za kukufanya ufanikiwe ili ndoto zako zifikie usipende kung’ang’ania vitu vinavyokutesa na kukuumiza na kuna uwezekano mkubwa unazuia mafanikio kuja kwako,”alisema Rose
Rose anasema kuwa hakuna mwanadamu ambaye alianza kutafuta maisha na kung’ang’ania kufanya kitu ambacho ni kigumu na kinamtia hasara bila kufikiria njia mbadala ya kujitatua, yeye kwa kutambua hilo hajabweteka kwa kuigiza tu, anajaribu kufanya kazi za ujasiriamali na pia anapenda kuwashauri wasanii wenzake wasing’ang’anie walipo tu.
Filamucentral