Siwezi Bila Seba- J Plus
MTAYARAISHAJI wa filamu Jimmy Mponda ‘Master’ amefunguka kwa kusema kuwa filamu za kimapigano anafanya vizuri anapokutana katika mapigano na mwigizaji Seba Mwangulo ‘Inspekita Seba’ ndio sababu anarudi naye tena.
“Sinema za action ni ngumu sana kucheza hasa ukikutana na msanii ambaye hajui sinema za mapigano, hivyo nimerudi na Ispekita Seba katika filamu The Foundation nimekubali uwezo wake,”
Wasanii hawa wawili walikutana katika filamu ya Misukosuko na kuifanya sinema kuwa gumzo kwa watazamaji na kuwajengea majina zaidi katika tasnia ya filamu Bongo ni kwa muda mrefu sasa wasanii hawa hawajakutana katika filamu.