Artists News in Tanzania

Snura: Majanga Ilinipa Majanga

STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Snura Mushi ambaye alipata kiki ya aina yake kwa kibao chake cha Majanga, amefunguka kuwa licha ya kupata shoo nyingi kupitia ngoma hiyo, lakini pia alipata majanga kwa kutapeliwa mara kadhaa.

snura-1

Snura Mushi

Akipiga stori na Risasi Vibes, Snura alisema promota mmoja alimpeleka kufanya shoo mkoani Kilimanjaro na Mererani Arusha, lakini baada ya kuwa ameshafanya kazi, mtu huyo alimkimbia bila kumpa chake, kiasi kwamba alilazimika kurejea Dar kwa lifti.

“Sitasahau, nilisaidiwa lifti mimi na wacheza shoo wangu kutuleta Dar, lakini baadaye nilikuja kumpata huyo promota, nikamnyang’anya pete ya ndoa na uchumba, ninazo mpaka leo maana hakunilipa,” alisema Snura.

Chanzo:GPL

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

 

Comments

comments

Exit mobile version