Artists News in Tanzania

Snura: Natamani Kufanya Shoo, Wimbo au Filamu na Shilole

MWANADADA anayetamba na ngoma ya ‘Shindu’ Mwaga Maji Tucheze Kama Kambare, Snura Mushi (pichani) ameeleza kiu yake ya kutaka kufanya kazi na mwanadada mwenzake Zuwena Mohammed ‘Shilole’ endapo atakuwa tayari.

Snura amebainisha hayo usiku wa Jumanne, Januari 24, 2017 wakati akijibu swali kwenye interview ya kipindi cha Redio EFM. Snura amesema kuwa  kwa sasa hana bifu kabisa na Shilole, hayo yalikuwa mambo ya zamani na yalisha kwisha kitambo na endapo ikitokea nafasi ya wawili hao kukaa chemba na kufanya kazi pamoja yuko tayari kwa asilimia zote.

“Kwa sasa sina bifu lolote na Shilole, tuko sawa, hayo yalikuwa mambo ya zamani sana tulishayamaliza, tupo sawa. Muziki wake na wangu uko tofauti hatuwezi kugombana”

“Kwanza natamani sana kufanya kazi pamoja na Shilole, ikiwezekana tufanye wimbo wa pamoja au movie (filamu) kwa kuwa yeye ni msanii mzuri wa kuigiza naamini tukifanya hiyo tutatengeneza pesa nzuri mimi na yeye”

“Kingine ni kwamba natamani pia kufanya naye shoo moja jukwaani hata kama ni hapa Dar es Salaam au popote, kwa maana sisi wasanii tupo kwa ajili ya kutafuta pesa, kwa hiyo ikitokea nafasi kama hiyo itakuwa poa sana.” Alisema Snura.

Mbali na hayo Snura hakusita kueleza jitihada zake za kumtafuta Shilole licha ya yeye kuonekana kama hayuko tayari kufanya hivyo.

“Nimewahi kumtafuta kwa jitihada zangu ili tuweze kufanya angalau jambo moja kati ya hayo (shoo, wimbo au filamu) lakini inavyoonekana mwenzangu kama hayuko tayari.” Alimalizia Shilole.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments

Exit mobile version