Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Steve Nyerere amesema anahitajika mtu wa kuweza kusimamia mambo ya maigizo, ngumi na michezo ya mpira ili kusogeza tasnia hizo na siyo watu wa kujiangalia wao binafsi.
Akiongea na eNewz Steve amesema hajaona kitu ambacho Eric Omondi anamzidi kwa kuwa kazi nyingi za Omondi huwa anakopi nyimbo za watu na ‘kujipromoti’ kwa nguvu ila hakuna Comedy yoyote ambayo anaifanya ya kumfanya Steve aweza kumuhofia.
Pia Steve amesema hamfahamu kabisa Eric Omondi kuwa ni nani kwenye sanaa ya Comedy hivyo ajaribu kufanya vitu vyake na siyo kukopi kwa wengine huenda akatambua kipaji chake.
eatv.tv
Comments
comments