Steve Nyerere: Mastaa Tupunguze ‘Raundi’
MCHEKESHAJI mahiri Bongo, Steve Nyerere amewataka mastaa wenzake kupunguza kuagiza raundi wanapokuwa kwenye starehe za unywaji pombe badala yake, siku moja moja wajitoe kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima.
Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na mfanyabiashara Davis Mosha nyumbani kwake Sinza, Steve aliwataka kuiga mfano wa pedeshee huyo kwa kuwa mara nyingi hujitoa kwa watoto yatima, kwani kwa kufanya hivyo, mambo yao mengi yatafunguka.
“Jamani tupunguze raundi wasanii wenzangu, badala yake tujitoe sana kwa watoto yatima maana ndugu yangu Davis siyo kwamba alilala na kuamka tajiri, yeye amekuwa akijitoa sana kwenye jamii isiyojiweza kama hivi,” alisema.
Chanzo:GPL