Artists News in Tanzania

Steve RnB Atoa Dongo kwa Nuruelly na Rama D

Msanii wa RnB nchini Steve RnB amesema hawezi kufanya muziki wa kisingeli na siku akifanya atachekesha hata Nuruelly na Rama D wamekosa washauri sahihi mpaka kuamua kufanya aina hiyo ya muziki.

Akipiga story ndani ya eNewz, amesema hadhani kama ni kitu sahihi kutoka katika muziki wa RnB na kuimba Singeli labda kama waliofanya hivyo walifanya kwa kutafuta mashabiki pamoja na kufanya mashabiki kumsikiliza kwa karibu kwa kuwa walikaa kimya kwa muda mrefu.

Hata hivyo alimsihi Nuruelly kutafuta washauri wazuri ili kuweza kufanya muziki mzuri kwa kuwa yeye anaamini kuwa Nuruelly anaweza akafanya muziki mzuri na ana sauti nzuri pia ni mtunzi mzuri sana wa nyimbo.

eatv.tv

Comments

comments

Exit mobile version