KIONGOZI wa Wasanii wa Vichekesho Tanzania, Habib Mkamba ‘Sumaku’ amesema kwamba kifo cha msanii mwenzao, James Peter ‘Kinyambe’ kilichotokea hivi karibuni, hakuna wa kuliziba pengo lake.
Akipiga stori na Ijumaa, Sumaku alisema Kinyambe alikuwa na staili yake ya kipekee katika uchekeshaji hivyo hakuna msanii anayeweza kuvaa viatu vyake.
“Mimi sijaona wa kuvaa viatu vya Kinyambe, pengo lake itakuwa vigumu kuzibika maana yule alikuwa na kastaili kake f’lani ka’ kuchekesha, ndiyo hivyo tena Mungu kamchukua,” alisema Sumaku.
Chanzo: GPL
Comments
comments