Msanii mkongwe wa filamu, Vincent Kigosi ‘Ray’ amesema filamu yake mpya ‘Tajiri Mfupi’ inakuja kuibua vipaji vipya vya kuigiza kutokana na ubora wake pamoja na wahusika aliyowatumia.
Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Ray alisema filamu hiyo itakuwa kubwa na itabadili mitazamo ya watu wengi kuhusu tasnia ya filamu.
“Tajiri Mfupi inatoka mwezi huu mwishoni,” alisema ‘Ni filamu kali kusema ukweli, itaibua vipaji vipya vya uigizaji kwa sababu ni kazi ambayo imeandaliwa kwa ubora mkubwa sana,”
Comments
comments