Tanzia: Mzee Tofi Afariki Dunia Tanga
MCHEKESHAJI Mahiri Salimu Athuman (Tofi) mwenye lafudhi ya Kichaga amefariki jana nyumbani kwake Duga Mwembeni mchana FC iliongea na Katibu wa TDFAA mkoa wa Tanga ndugu Raphael William Kiango na kudhitisha kifo hicho kwa mujibu wa familia yake.
“Mzee wetu msanii mwezetu Tofi amefariki mchana akiwa nyumbani kwake na likuwa akisumbuliwa na ugonjwa Kansa ya koo na mwili wake umeifadhiwa katika Hospitali ya Bombo anazikwa leo saa kumi jioni,”Katibu Kiango anasema.
Msanii huyo nyota aliyejizolea umaarufu katika kipindi cha Vunja Mbavu akiwa sambamba na King Majuto pamoja na kipindi cha sasa Vituko show ameacha mke na watoto saba, Tofi alikuwa mahiri sana katika kuongea kama Mchaga anatarajia kuzikwa katika makaburi ya Duga Maforoni Tanga.